Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Arusha imemwachi huru na kufuta shitaka la aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha, Lengai Ole Sabaya aliyekuwa anakabiliwa na shitaka la kujifanya mtumishi wa umma katika idara ya usalama wa taifa (TISS)

Mahakama imefuta shitaka hilo baada ya upande wa Jamhuri kuliondoa shitaka hilo mahakamani kwa mara ya nne mfululizo hivyo kuona haina haja ya kuendelea nalo.

Wakili wa Serikali, Pernina Joakimu ameiambia mahakama mbele ya Hakimu Mkazi, Nestory Barro kuwa upande wa Jamuhuri umeona hakuna haja ya kuendelea na shitaka hilo hivyo anaiomba mahakama ilifute.

Aidha, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya mkoa wa Arusha, Nestory Barro ameutaka upande wa Jamuhuri kupitia wakili huyo wa serikali kuacha tabia ya kupeleka shitaka mahakamani na kulitoa kwakuwa ni kinyume na haki za binadamu huku akimtaka wakili wa serikali kusoma vipengele vya sheria vinavyo ainisha ukomo wa mtu binafsi au taasisi yoyote kumsumbua mtu.

Hata hivyo, akizungumza nje ya Mahakama hiypo mara baada ya kufutiwa shtaka hilo, Lengai Ole sabaya ambaye pia ni diwani wa kata ya Sambasha kwa tiketi ya CCM amesema anaishukuru mahakama kwa kumpa haki kwakuwa yote hayo yanatokana na chuki za kisiasa

Serikali kuanza kupiga mnada mali za wadaiwa sugu
Amber Lulu atiwa mbaroni kwa makosa ya kimtandao