Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa miongoni mwa sababu za yeye kuiongoza Dar es salaam ni kuhakikisha wananchi wa Mkoa huo wanapona kupitia yeye, kwa namna ambavyo amekuwa akijitolea mara kwa mara kuhusu suala la tiba.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kupona kwa kijana aliyekuwa akiugua maradhi ya kansa ya jicho, Ashraf Patrick ambaye kwa sasa amepona baada ya kupata msaada kutoka kwake.

“Mungu alijua kwanini nimekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, ili nikae karibu na Muhimbili ili wananchi wapate huduma, wawe sehemu ya mafanikio ya matibabu na uponyaji wa watoto wengi masikini,” amesema Makonda.

Amesema kuwa shraf sasa anarudi Bukoba akiwa na furaha tele, baada ya kupona hivyo amewashukuru waandishi wa habari kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa kwenye mkoa wa Dar es salaam.

Aidha, Makonda amekiri kuwepo kwa kwa baadhi ya watu ambao wanashindwa kumudu gharama pindi wanapokuwa wakipata matibabu kwenye hospiali na amesema wao kama mkoa watahakikisha wanaandaa mpango wa kuwasaidia watu hao.

Mama Samia akanusha taarifa za Urais
Stars yaanza maandalizi kuichakaza Burundi Kuelekea kombe la Dunia