Gwiji wa soka duniani Diego Armando Maradona Franco, ameapa kupigana usiku wa mchana ili kumaliza vimelea vya rushwa ambavyo anaamini bado vipo ndani ya shirikisho soka ulimwenguni FIFA.

Maradona ambaye alionekana kumpinga wazi wazi Sepp Blatter wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwezi Mei mwaka huu, amesema pamoja na uchunguzi kuendelea kufanywa kwa baadhi ya maafisa wa FIFA, anaamini kuna masalia ya watu ambao walikuwa wakifanya biashara haramu.

Gwiji huyo wa soka kutoka nchini Argentina, amesisitiza kuwa mstari wa mbele kwenye mchakato wa kupigania jambo hilo na ana imani atafanikiwa kutokana na kuchukizwa na namna soka linaendelea kuchafuliwa kwa tamaa za watu wacheche.

Hata hivyo amedai kwamba anatambua kuna wadau wa soka wanahitaji kumsaidia lakini ni vigumu kwao kujitokeza hadharani, ila amesisitiza kuwa nao bega kwa bega ili kulimaliza tatizo ambalo linapoteza muelekea na maana ya mchezo wa soka.

Kwa kipindi kirefu Diego Maradona amekua akithubutu kuonyesha dhamira ya kupigania ukweli kwa kuamini analinusuru soka ambalo linastahili kuwasaidia vijana wanaochipukia kwa sasa ili liweze kuwanufaisha kama ilivyokua wakati akiwika duniani miaka ya 1980-90.

Dkt Slaa Akanusha Yaliyosambaa Kuhusu Yeye, Lowassa Na Chadema
Lowassa Na Lissu Wachochea Kuni Wakati Wa Kuchukua Fomu