Mchungaji mmoja nchini Afrika Kusini, Alfred Ndlovu ameripotiwa kufariki kwa njaa kali na kiu baada ya kuingia kwenye mfungo mkali bila kugusa chakula akiwa na nia ya kuvuka siku 40 alizofunga Yesu Kristo.

Taarifa kutoka nchini humo zimeeleza kuwa mwili wa mchungaji huyo ulikutwa msituni baada ya siku 30, alikoenda kufunga bila kubeba chakula chochote, akiwaahidi waumini wake kuwa atafunga zaidi ya siku 40 alizofunga Yesu Kristo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Buzzsouthafrica, Mchungaji huyo aliondoka nyumbani kwake Juni 17, lakini baada ya ukimya wa muda mrefu mtu mmoja alibaini mwili wake msituni na kutoa taarifa polisi waliouchukua.

Waumini wake wamemtaja kama mtu aliyekuwa mcha Mungu sana na aliishi maisha ya kiroho kwa imani kubwa ‘ya kuhamisha milima’.

“Alikuwa mtu wa imani. Ni bahati mbaya amekumbwa na kifo cha njia hiyo. Baada ya mwezi mmoja kupita tulipata habari ya kusikitisha kuhusu kifo chake,” alisema mmoja wa ndugu zake wa karibu.

Video: BASATA yawatahadharisha wasanii kusoma alama za nyakati, kufuata sheria
Breaking News: Ndege ya Emirates yaanguka ikiwa na abiria 275