Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba amesema mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa alitaka kukihama chama hicho tangu mwaka 1995 lakini alimshauri kutofanya hivyo.

Akiongea katika mkutano wa CCM mjini Morogoro, mzee Makamba alisema kuwa mwaka 1995, Halmashauri Kuu ya chama hicho ililikata jina la Edward Lowassa baada ya kutilia shaka utajiri mkubwa aliokuwa nao akiwa na umri mdogo. Alisema la Lowassa halikuchaguliwa kuwa kati ya makada watano waliopitishwa na Kamati Kuu katika mchakato wa kumpata mgombea urais ambapo Benjamin Mkapa aliibuka mshindi .

Alieleza kuwa baada ya hatua hiyo, Lowassa aliongea na Mzee Makamba na kumuuliza ushauri kama anayo sababu ya kuendelea kukaa katika chama hicho.

“Aliniuliza, ‘mzee Makamba bado nina haja ya kubaki CCM?’, nikamwambia ukihama utakuwa umeruka matope umekanyaga mavi,” alisema.

Mzee Makamba alieleza kuwa Edward Lowassa alimsikiliza na kuendelea kuwa mwanachama wa CCM hadi alipoamua kukihama chama hicho mwaka huu.

Magufuli Kuwanyang’anya Mashamba Wawekezaji
Wananchi Waibadilikia CCM