Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) imechambua rufaa zingine 34 za ubunge, ambapo kati ya hizo, tume imewarejesha wagombea 13 na kuwakataa wagombea 21.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa uchaguzi Dkt. Wilson Mahera leo Septemba 9, 2020, rufaa hizo 13 zinahusu majimbo ya Singida Magharibi, Madaba, Ilemela, Namtumbo, Bagamoyo, Liwale, Tunduma, Bukene na Kigamboni.

Dkt. Mahera amesema NEC imekataa rufaa saba za wagombea ambao hawakuteuliwa kutoka majimbo ya Singida Magharibi, Bahi, Handeni vijijini, Madaba,Singida Mashariki, Ileje , Meatu na Bukene.

Amesema, tume hiyo baada ya uchambuzi imekataa rufaa 14 za kupinga walioteuliwa kutoka majimbo ya Mwanga, Mafinga, Ilala, Manonga, Igunga na Kisesa.

Jana Septemba 8, NEC ilianza kutoa majibu ya rufaa zilizoshugulikiwa ampapo ilitangaza maamuzi ya rufaa 55 na kufanya idadi ya rufaa zilizoshughulikiwa mpaka sasa kufikia 89.

Maalim Seif atakavyopambana na wanaompinga
Ronaldo aweka rekodi mpya Ureno