Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli imetoa onyo kali kwa madaktari wote wanaojihusisha na biashara haramu ya kuwatoa ujauzito wanawake na wanafunzi.

Akizungumza katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma alipofanya ziara na kujionea hali halisi ya utoaji huduma ya afya kwa wananchi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa atawafukuza kazi na kuwafunga jela madaktari ambao wanadaiwa kuwa maarufu kwa kuwatoa mimba wanawake kinyume cha sheria.

Waziri Mkuu alisema kuwa anafahamu kuwa hospitali hiyo ya mkoa wa Ruvuma inasifika kwa utoaji mimba na waliotolewa hulazwa katika wodi namba 5. Alisema tayari anayo majina ya madaktari wanaotuhumiwa kufanya vitendo hivyo.

“Naomba mkuu wa mkoa fanya ziara ya kushtukiza katika wodi namba 5 utakuta wanawake wametolewa mimba, wakiwemo wanafunzi na kisha madaktari hao wanatumia wodi zetu kuwalaza wagonjwa wao waliowatoa mimba.Ni marufuku na nitawachukulia hatua kwani majina ya madaktari hao ninayo,” alisema Waziri Mkuu.

Aliwataka Mganga Mkuu na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo kuwafuatilia madaktari hao wanaowatoa mimba akina mama na wanafunzi.

Ronaldo De Lima Amkubali Messi Kuliko Wajina Lake
Hiddink Hajaridhishwa Na Uchezwaji Wa Chelsea