Mshambuliaji kutoka Ufaransa Olivier Giroud ametuma salamu kwa waajiri wake wa zamani (Arsenal), baada ya kuisidia Chelsea kutinga hatua ya fainali kombe la FA England.

Giroud aliifungia Chelsea kwenye ushindi wa mabao matatu kwa moja  dhidi ya Manchester United katika mchezo wa hatua ya nusu fainali na lilikuwa bao lake la nane katika mechi 21 alizocheza kwenye michuano yote msimu huu.

Arsenal walitangulia fainali kwa kuibanjua Manchester City mabao mawili kwa sifuri siu ya Jumamosi, mabao ya Washika Bunduki hao yakifungwa na na mshambuliaji kutoka Gabon Pierre-Emerick Aubameyang.

Giroud, ambaye ataingia uwanjani kusaka taji lake la pili la Kombe la FA akiwa na Chelsea, amesema anasubiri kwa hamu kubwa kukabiliana na waajiri wake hao wa zamani.

Giroud alijiunga na Arsenal mwaka 2012, mahali ambako alishinda mataji matatu ya Kombe la FA kabla ya kuuzwa Chelsea, Januari 2018 kumpisha Pierre-Emerick Aubameyang huko Emirates.

“Niliwaambia vijana nataka kushinda tena taji hili, litakuwa taji langu la tano la Kombe la FA na tumeshafika fainali. Mchezo dhidi ya Arsenal utakuwa maalumu kwangu binafsi.”

“Tumekuwa tukicheza vizuri na mpango wetu ni kumaliza kwenye tatu bora katika Ligi Kuu England.”

Licha ya kujiunga Chelsea, Giroud bado amekuwa akiheshimika na mashabiki wa Arsenal, lakini aliwatibua baadhi ya mashabiki hao baada ya kushangilia kwa staili ya kuwakejeli kwenye fainali ya Europa League msimu uliopita.

Giroud aliwafunga Arsenal kwa kichwa katika fainali hiyo iliyofanyika mjini Baku na mashabiki wa Arsenal wamekuwa na mashaka makubwa huenda akarudia kuwafunga kwenye fainali ya Kombe la FA.

Magufuli akerwa TAKUKURU kupendelea Chato, "mtanivuruga"
Matokeo Majimbo mengine 70 kura za maoni CCM