Mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, aliutikisa mji wa Musoma kwa siku mbili mfululizo huku akivunja rekodi ya ‘mbwembwe’ za kisiasa zilizofanywa na wafuasi wa chama hicho, pamoja na umati wa watu waliofurika kumuona.

Ripoti kutoka mjini hapo zinaeleza kuwa, Lowassa aliingia mjini hapo jana jioni na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa wafuasi wa chama hicho ambao walimsindikiza hadi kwenye hotel aliyofikia.

Hata hivyo, msafara mkubwa wa wafuasi hao wa Chadema uliingia dosari baada ya polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya. Hata hivyo, wafuasi hao walionekana kwenye mitaa hiyo na wengine walilala nje ya hotel aliyofikia iliyopo katikati ya mji huo, kwa kile walichodai kumlinda ‘rais wao ajaye’.

Lowassa Muosma 2

Mapema asubuhi (Oktoba 11), umati mkubwa ulifika katika eneo la hoteli hiyo na kumsindikiza hadi kanisani la KKKT – Usharika wa Nyasho, alipoenda kuhudhuria ibada, kisha alianza safari ya kuelekea katika kijiji cha Bukima, Musoma Vijijini ambako alifanya mkutano uliohudhuriwa na umati wa watu.

Wananchi Wa Musoma Mjini wakiusindikiza msafara wa Edward Lowassa

Wananchi Wa Musoma Mjini wakiusindikiza msafara wa Edward Lowassa

Moja kati ya vivutio, ni wafuasi hao kamua kudeki mababara yote ya lami na kufanya usafi wakidai kuwa wanamsafishia njia na mazingira ‘rais wao ajaye’.

Wadeki Barabara

msm

Majira ya mchana mji wa Musoma uligeuka kuwa wa rangi za Chadema ambapo wakazi wa mji huo walimiminika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mukendo kwa ajili ya kumsikiliza mgombea huyo. Na mara alipowasili katika uwanja huo, ilimchukua takribani dakika 30 kufika katika jukwaa kuu kutokana na msongamano wa watu, huku vijana wakiwa wanalifuta gari lake kwa kutumia mashati yao.

Lowassa Musoma 2

Baada ya viongozi wa Ukawa, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye pamoja na mbunge wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere kuhutubia, hatimaye, Lowassa aliwahutubia wananchi wa jimbo hilo huku wakiwa wanashangilia muda wote.

Lowassa aliwahidi wananchi hao kuwa akichaguliwa kuwa rais atahakikisha anaifufua bandari ya Musoma, kufanikisha ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Mwalimu Nyerere jimboni hapo pamoja na kukamilisha ujenzi wa hospital ya rufaa iliyoko katika eneo la Kwangwa, mjini hapo.

“Tutamalizia ujenzi wa bandari ya Musoma na itakuwa ya kisasa…kuna hili suala la chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere, nitalifuatilia hapa na mbunge tuhakikisha kinaanzishwa. Lakini pia ile hospitali ya rufaa tutaikamilisha katika kipindi cha miaka mitatu itakua inatoa huduma,”alisema.

3musoma

Katika hatua nyingine, mgombea huyo alionesha kusikitishwa kwake na vitendo vya wafuasi wa chama hicho kupigwa mabomu ya machozi na polisi. Aliwataka polisi kutowapiga wananchi mabomu ya machozi katika kipindi hiki, na kwamba wanaweza kujikuta wakifikishwa kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ‘ICC-The Hegue’.

Mgombea huyo anaendelea na kampeni zake katika kanda ya ziwa ambapo kesho atakuwa katika jimbo la Bunda Mjini, linalowaniwa na Esther Bulaya (Chadema) na Stephen Wasira (CCM).

CCM Yaahidi Neema Mpya Kwa Wafanyabiashara Wadogo
Mengi Akanusha Taarifa Zilizosambazwa Kuhusu Yeye Na Lowassa