Edward Lowassa, mgombea urais kupitia Chadema anaeungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, leo amelazimika kusimama na kuwahutubia maelfu ya wakazi wa Muheza, Tanga waliojipanga barabarani.

Taarifa kutoka Muheza zinaeleza kuwa walizuia msafara wa Lowassa kwa mbwembwe huku wengine wakidaiwa kulala barabarani wakimtaka mgombea huyo kuwahutubia kabla hajapita eneo hilo.

LWS

Lowassa alikuwa akitokea Tanga Mjini ambapo jana alifanya mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na mafuriko ya watu waliouzidia uwanja wa Tangamano na kumlazimu kuahirisha mkutano huo ili kunusuru maisha ya watu walioanza kupoteza fahamu uwanjani hapo.

lws 4

Mgombea huyo ameonekana kubebwa na jiji la Tanga na wilaya zake hivyo kuacha alama za kuuliza endapo jiji hilo bado lina sifa za kuendelea kuitwa ngome ya CCM.

Wakazi wa Korogwe wakimsikiliza Lowassa

Wakazi wa Korogwe wakimsikiliza Lowassa

Msingwa Na Wafuasi Wa Chadema Watupwa ‘Selo’
Blatter, Platini Watangaza Misimamo Yao