Ushabiki wa kisiasa uliovuka mipaka umepelekea kifo cha Mwalimu wa Shule ya Sekondari Manushi Kibosho, wilani Moshi Vijijini, aliyetajwa kwa jina la Demetus Dastan, anaesadikika kuwa alipigwa na mfuasi wa Chadema kwa madai ya kuchana picha ya mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani, mwili wa marehemu ulikutwa katika shamba la mwanakijiji aliyetajwa kwa jina la Joachim Massawe ukiwa na majeraha katika sehemu mbalimbali.

Taarifa hizo zilieleza kuwa, masaa machache kabla ya kifo chake, marehemu alikuwa katika klabu moja kijini hapo akinywa pombe ambapo ulizuka ubishani wa kisiasa uliopelekea ugomvi wa ngumi kati yake na mtu mwingine uliotokana na kuchanwa kwa picha ya Edward Lowassa.

Baada ya ugomvi huo, marehemu aliondoka na kuelekea nyumbani kwake ambapo hakuonekana hadi mwili wake uliopokutwa shambani hapo.

Kompany: Hatuihofii Juventus
Kikwete: Nitamtaja Mwenye Richmond