Klabu ya Chelsea imekamilisha usajili wa Kiungo Mshambuliaji kutoka England Chukwunonso Tristan “Noni” Madueke, akitokea PSV Eindhoven ya Uholanzi kwa ada ya Pauni milioni 30.7.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amekamilisha taratibu zote za kujiunga na The Blues leo Jumamosi (Januari 21), akisaini mkataba wa miaka saba na nusu, ambao una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Madueke anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa Chelsea katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo akitanguliwa na Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ukraine Mykhailo Mudryk aliyeigharimu The Blues Pauni Milioni 89 siku tano zilizopita.

“Nimefurahishwa sana kusajiliwa na moja ya klabu bora zaidi duniani,” Madueke aliambia tovuti ya Chelsea

“Kurejea Uingereza na kucheza Ligi Kuu ni ndoto kwangu na familia yangu na siwezi kusubiri kuanza.”

“Nina furaha kwa siku zijazo, ninatarajia kupambana kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu ili kushinda mataji nikiwa hapa.”

Madueke alipitia mfumo wa vijana katika Klabu ya Crystal Palace na Tottenham kabla ya kuondoka Uingereza na kuhamia Uholanzi akijiunga PSV mwaka 2018.

Alifunga mabao 21 katika mechi 77 alizoichezea Uholanzi, lakini upande wa kikosi cha England chini ya miaka 21 amecheza michezo minne pasina kufunga bao.

Aliyepora shamba avamiwa na nyuki
Young Africans yarudishwa Gym