Mtoto wa mshambuliaji waliyewahi kuwika na klabu za AC Milan, FC Barcelona pamoja na timu ya taifa ya Brazil, Rivaldo Vítor Borba Ferreira ameelekea barani Ulaya kuanza maisha mapya ya soka lake.

Rivaldinho, mtoto wa mshambuliaji huyo ambaye bado anasakata kabumbu huko nchini kwao Brazil, amekamilisha usajili wa kuitumikia klabu ya Boavista ya nchini Ureno.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 20, amejiunga na klabu hiyo ya nchini Ureno, akitokea nchini kwao Brazil alipokua akiitumikia Mogi Mirim inayoshiriki ligi daraja la pili.

Uongozi wa klabu ya Boavista ulithibitisha kumnasa Rivaldinho kupitia tovuti yao usiku wa kuamkia hii leo, huku ukijinasibu kumpata mchezaji ambaye atamaliza kiu ya upachikaji wa mabao klabuni hapo.

Baba wa Rivaldinho, mwenye umri wa miaka 43, alionyesha furaha yake kupitia mtandaio wa Instagram kwa kuandika “Mungu Amesekia Dua Zangu Kwa kumuwezesha Mwanangu Kuelekea barani ulaya Kucheza Soka Kwa Mafanikio Zaidi, Naihakika Mungu Ataendelea Kumsaidia”.

Wakati baba akiandika maneno hayo, Rivaldinho akaongezea katika mtandao Instagram kwa kuandika “Nimefarijika Kupata Mahala Pengine Pa Kucheza Soka Langu, Sina Budi Kuwashukuru Wote Waliofanikisha Hili Na Ninaahidi Sitowaangusha”.

Akiwa kwenye klabu ya Mogi Mirim, Rivaldinho alifanikiwa kucheza mkichezo 47 na kufunga mabao 11.

Mabango Ya Wagombea Marufuku Vituo Vya Mabasi Dar
Hali Tete kwa Twiga Stars