Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, imepanga Oktoba Mosi mwaka huu, kutoa hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai ole Sabaya na wenzake wawili.

Hayo yamejiri baada ya washtakiwa hao kumaliza kujitetea leo Agosti 24, 2021, ambapo washtakiwa hao walikuwa wakitetewa na mawakili sita Dancan Oola,Mosses Mahuna,Edmund Ngemela,Sylvester Kahunduka,Fridolin Gwemelo na Jeston Jastin.

Hata hivyo kwa Upande wa Jamhuri ulioita mashahidi 11 ulikuwa ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu,Tumaini Kweka,wakili Mwandamizi Abdalah Chavula, na Mawakili wa Serikali Felix Kwetukia na Baraka Mgaya.

Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, amekubali maombi ya mawakili wa pande zote mbili walioomba kufanya majumuisho kwa njia ya maandishi kwa muda wa siku saba.

Katika Kesi hiyo, Sabaya na wenzake wawili wanatuhumiwa Kwa makosa matatu ya unyang’anyi wa kutumia silaha katika duka la Mohamed Saad lililopo eneo la bondeni jijini Arusha Februari 9 mwaka huu.

TBS kuboresha mafunzo ya ithibati
Simon Patrick aikingia kifua Young Africans, amjibu Jemedari Said