Hatimaye Mshambuliaji kutoka Ghana Michael Sarpong amerudishwa kwenye kikosi cha Young Africans kuendelea na mazoezi sambamba na wachezaji wenzake.

Kikosi cha Young Africans kwa sasa kinajiandaa na michezo miwili ya mwisho ya Ligi Kuu Tanzania Bara (Ihefu FC na Dodoma Jiji FC) pamoja na mchezo wa Fainali Kombe la Shirkisho *ASFC* utakaochezwa mkoani Kigoma Julai 25, Uwanja wa Lake Tanganyika.

Sarpong alisimamishwa na Uongozi wa Young Afrivans baada ua kupokea taarifa za utovu wa nidhamu alioufanya kutoka kwenye benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Nabi.

Baada ya kikao walichokutana juzi Viongozi pamoja na Kocha Nabi kambini Avic Town, kwa pamoja wameamua kumrudisha kundini mshambuliaji huyo.

Wachezaji wengine ambao bado wapo nje ya kikosi cha Young Africans kwa sababu za utovu wa nidhamu ni Kiungo kutoka Rwanda Haruna Niyonzima na Beki Kutoka Ghana Lamine Moro.

Angel Di Maria: Messi alinishukuru kwa furaha
Ahadi zamiminika Raja Casablanca