Msemaji mkuu wa serikali Dokta Hassan Abbas amesema fedha zote za miradi ya serikalib zipo kwenye bajeti, zinazpitishwa Bungeni kila mwaka na hakuna usiri wowote.

Abbas ametoa kauli hiyo katika mahojiano na chombo kimojawapo cha habari ambapo amesema fedha za miradi yote inayotekelezwa nchini zipo na zimetengwa kwa mujibu wa sheria na kwamba miradi hiyo imelenga kuboresha maisha ya watanzania.

Sambamba na hilo, dokta Abbas amezungumzia madai ya ndege kununuliwa kwa siri bila bajeti na kusema ununuzi ulifanywa kwa mujibu wa kifungu cha sheria 65A cha ununuzi wa umma.

“Kama kuna mtu alikuwa na wakala wake mfukoni katika ununuzi wa hizi ndege imekula kwake, serikali imenunua moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji wanaojulikana kimataifa kama boeing na Bombardier na sheriainaruhusu hivyo na ilipata bei ya chini kuliko hata zilie zilizoainishwa kwenye tovuti zao” amesema Abbas.

Hivi karibuni, mgombea urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu akiwa katika moja ya mikutano yake ya kampeni alisikia akiishutumu serikali juu ya fedha ilizozitumia ndege hizo.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 25, 2020
Uchaguzi usiwe chanzo cha uvunjifu wa amani nchini - Lipumba

Comments

comments