Wagonga Nyundo wa Jijini London (West Ham Utd) wameanza mchakato wa kumsaka mbadala wa Slaven Bilic, ambaye anakabiliwa na mtihani wa kwenda sambamba na malengo ya klabu hiyo.

The Hammers wamethibitisha kuwa katika mpango huo, kwa kumpa masharti Bilic ya kuhakikisha anamaliza msimu katika nafasi kumi za juu, kinyume na hapo wataachana nae.

Bilic, amekua katika masukumo wa kutakiwa kufanya vizuri ili asainishwe mkataba mpya, lakini hali inaendelea kuwa mbaya dhidi yake kutokana na kikosi cha West Ham Utd kushindwa kuo9nyesha umahiri wa ushindani dhidi ya timu pinzani.

Tetesi zilizoandikwa katika baadhi ya vyombo vya habari nchini England hii leo zimedai kuwa, huenda nafasi ya Bilic ikajazwa na aliyekua meneja wa Man City Roberto Mancini ambaye kwa sasa hana kazi.

West Ham Utd ipo katika nafasi ya katika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi ya nchini England kwa kufikisha point 33, na imesaliwa na michezo 12.

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (KJCI) yatoa neno kwa Rais Magufuli
Wakenya watamani nchi yao iwe kama Tanzania