UTI (Urinary tract infection) ni ugonjwa wa maambukizi katika mfumo wa mkojo na maambukizi haya yanasababishwa na viumbe kama bakteria, fangasi na virus.

Mara nyingi bakteria wanaoingia kwenye mfumo wa mkojo hutolewa na mwili, Wakati mwingine bakteria hawa wanazidi kinga ya mwili na kusababisha maambukizi hayo.

UTI inaweza kuathiri  viungo kama urethra, kibofu cha mkojo na figo.

UTI zinasababishwa na bakteria aitwaye Escherichia coli (E. coli) na nyingine zinasababishwa na Chlamydia na Mycoplasma UTI hizi zina athiri hadi mfumo wa uzazi na wanandoa wanapaswa kupata tiba pamoja.

Maambukizi ya UTI ni makubwa sana duniani zaidi ya watu milioni 8.1 wanaathiriwa na ugonjwa huu.

Hizi ni njia ambazo mwanamke anashauriwa kuzifanya ili kujikinga na kupata maambukizi ya ugonjwa wa huu.

  1. Kukojoa baada ya tendo la ndoa

Kwa kufanya hivyo husaidia kuondoa bakteria na vijidudu vingine vya magonjwa ambavyo vinaweza kuwa viliingia kwenye mrija wa mkojo wakati unashiriki tendo la ndoa.

2. Kujisafisha kutoka mbele kwenda nyuma

Hii inafanyika kila baada ya haja kubwa na ndogo kwani inasaidia kuzuia uingiaji wa bakteria ndani ya mrija wa mkojo kupitia uke, kwa kufanya hivyo utakuwa umejikinga na ugonjwa huu wa UTI ambao umekuwa sugu siku za hivi karibuni.

3. Kutoa haja ndogo ukiwa umetulia

Mara nyingi kujisaidia huku umesimama au umejikunja kwa nmana yeyote ile hubana misuli ya kibofu cha mkojo hivyo husababisha kiasi fulani cha mkojo kibaki ndani, hii husababisha athari kwenye kibofu cha mkojo pamoja na magonjwa hasa UTI, wakati wa haja ndogo jitahidi uchuchumae au ukae .

4. Hakikisha mkojo wote unatoka

Hakikisha huutunzi mkojo kwa muda mrefu unapofanya hivi wadudu hasa bakteria huzaliana kwa wingi, unajiweka kwenye hatari ya kuugua magonjwa hasa UTI.

Mbali na hayo yote, inashauriwa mtu kuhakkisha anavaa nguo za pamba na zile zilizokauka na ambazo hazikubani sana ili kuruhus hewa kupika.

Diamond aitika wito wa serikali
Hali tete Rukwa Wanafunzi wa Sekondari wawapa Mimba wa Msingi