Licha ya kutocheza mchezo wowote  kwa zaidi ya mwezi mmoja, Tanzania imepanda tena kwenye viwango vya ubora wa soka vya FIFA.

Shirikisho la soka la kimataifa, FIFA, limetoa viwango vipya vya soka vya mataifa wanachama wake kwa mwezi wa pili.

Katika viwango hivyo, Tanzania imepanda nafasi moja juu kutoka nafasi ya 126 duniani mwezi uliopita hadi  nafasi ya 125.

Kwa upande wa nchi za CECAFA, Uganda inaongoza licha ya kuporomoka nafasi 8 Duniani kutoka nafasi ya 63 hadi nafasi ya 70.

Rwanda ni ya pili kwa CECAFA baada ya kupanda kwa nafasi sita  duniani na kutua katika nafasi ya 85 ikifuatiwa na Kenya katika nafasi ya 99.

Hakuna mabadiliko katika nafasi ya juu, Ubelgiji ikiendelea kuongoza duniani. Kwa upande wa Afrika, Ivory Coast bado wanaoongoza barani Afrika licha ya kuporomoka kwa nafasi tisa.

Mbeya City Waibanjua JKT Ruvu
Malale Hamsini Aendelea Kuzigonganisha JKU, Ndanda FC