Rais wa Marekani, Donald Trump amefanya maamuzi ya kihistoria ya kupindua sera za miaka mingi za Marekani kwa kuutangaza mji wa Yerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Trump ametangaza kuwa Ubalozi wa Marekani utahamishwa kutoka mji wa Tel Aviv kwenda Yerusalem, ambapo amesema kuwa uamuzi huo haulengi kujiondoa kwa Marekani katika juhudi zake za kuleta amani katika eneo hilo la mashariki ya kati.

“Uamuzi huu haulengi kujiondoa kwa Marekani katika juhudi zake za dhati za kuleta amani ya kudumu bali inataka kutafuta suluhu ya mgogoro wa miaka mingi kati ya Israel na Palestina ambao Marekani haifungamani na upande wowote na kuingilia mipaka ya Israel na mamlaka zake ,na hatuko tayari kuingilia katika migogoro yao ,hayo ni mambo yao wenyewe,”amesema Trump

Kwa upande wake Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas amesema kuwa amesikitishwa na maamuzi ya Rais Trump na kudai kuwa Marekani imepoteza haki ya kusimamia hatua ya kupatana kwa amani ambayo imekuwa ikitafutwa miongo kadhaa iliyopita.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Natanyau ameunga mkono hatua ya Rais Trump na kusema kuwa ni maamuzi ya kihistoria licha ya kuwa Wapalestina wamemkosoa na huku Uingereza na nchi nyingine wanachama wa baraza la usalama wa umoja wa mataifa wameitisha kikao cha dharura ili kujadili maamuzi hayo.

 

Vigogo kukutana hatua ya mtoano Ulaya
Spartak Moscow wabebeshwa kapu la magoli Ulaya