Uongozi wa klabu ya Valencia, umeonyesha kuwa tayari kuingilia kati mipango ya klabu ya Man Utd, ambayo inatajwa kumshawishi meneja kutoka nchini Ureno Jose Mourinho, ili akubali kujiunga nao mwishoni mwa msimu huu.

Valencia wameanza kuingia katika harakati hizo, kufuatia maamuzi waliyoyachukua jana jioni ya kumtimua kazi aliyekua meneja wao kutoka nchini England, Gary Neville, ambaye alionekana kushindwa kufaulu mtihani wa kupata matokeo mazuri tangu alipoajiriwa mwanzoni mwa mwaka huu.

Mapema hii leo gazeti la The Sun la nchini England limeibuka na kichwa cha habari kilichosema “Forget Man United — come and join us now!” (“Isahau Man United — njoo ujiunge nasi!”) na chini yake kuna picha ya Jose Mourinho.

Gazeti hilo limeibuka na taarifa hiyo, huku ikifahamika kwamba Mourinho amekua akihusishwa na mipango ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Man Utd kupitia kwa wakala wake Jorge Mendez.

Hata hivyo fununu zilizopo zinadai kwamba, wakala huyo wa Jose Mourinho, amekua na mahusiano ya karibu na mmiliki wa klabu ya Valencia, Peter Lim, hivyo huenda ikawa rahisi kwao kuubadili upepo wa mazungumzo anayoyafanya huko Old Trafford.

Mourinho, aliwahi kuhusishwa na taarifa za kutaka kujiunga na klabu ya Valencia mwishoni mwa mwaka 2015, siku chache baada ya kuondoka Chelsea, na mazungumzo yalikua yameshaanza kati ya pande hizo mbili huku Mendez akihusika kwa asilimi 100, lakini mambo yalikwenda marama na ahadi iliwekwa ya kuyazindua tena itakapofika mwezi Februari mwaka huu.

Mmiliki wa klabu ya Valancia, Peter Lim amekua na shauku ya kutaka kuiona klabu hiyo ikifanya vyema katika ligi ya nchini Hispania kama ilivyo kwa klabu za Real Madrid pamoja na FC Barcelona na aliamini kuajiriwa kwa Gary Neville, kungeleta mabadiliko hayo.

Taarifa za awali zinadai kwamba kibopa huyo raia wa Singapore, amemtayarishia Jose Mourinho kiasi cha pauni million 15 kama mshahara wake kwa mwaka sambamba na pauni million 100 kwa ajili ya kufanya usajili.

Viongozi Wa Stand Utd Waufyata Kwa Patrick Liewig
Charles Boniface Mkwasa Anadai Mamilioni Ya Shilingi