Mashabiki lukuki wa klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki, wamemlaki kwa shangwe mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi, Robin van Persie.

Van Persie, amewasili mjini Istanbul, baada ya viongozi wa klabu ya Man Utd kukubaliana na wenzao wa klabu ya Fenerbahce na sasa kinachosubiriwa ni harakati zingine za kukamilishwa kwa usajili wake.
Hii leo, mshambuliaji huyo ambaye alisajiliwa na Man Utd akitokea Arsenal mwaka 2012, anatarajia kufanyiwa vipimo vya afya, na kama mambo yatakwenda vizuri atakamilisha mpango wa kucheza soka nchini Uturuki msimu ujao wa ligi akiwa na klabu ya Fenerbahce.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, aliwasili mjini humo akiwa sanjari na familia yake ya watoto wawili.
Akiwashukuru mashabiki waliojitokeza kumlaki, Van Persie alisema amejisikia faraja na anaamini ukaribu wao hautoishia hapo bali utaendelea hadi uwanjani katika kusaka mafanikio ya klabu hiyo ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya nchini Uturuki.

Tayari klabu ya Fenerbahce, imeshamsajili mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Ureno, Luis Nani ambaye msimu uliopita aliitumikia klabu ya Sporting Lisbon akitokea Man Utd kwa mkopo.

Mourinho Amtumia Fabregas Kushawishi Pedro
Peter Schmeichel Kufanya Kazi na Mwanae