#SAUTI ZETU ya Dar24 inakukutanisha moja kwa moja na msanii Omary Niyonzima anayefanya kazi zake za muziki nchini Canada. Omary Niyonzima (Papa Fololo) ni Mtanzania kutoka katika familia ya mzee Ally huko Uvinza, Kigoma ambaye aliimbia Band mbali mbali za muziki kama TOT na nyingine, hivi sasa anaishi nchini Canada akifanya muziki wa asili ya Tanzania (muziki wa pwani), Taarabu ambapo ameeleza kuwa malengo yake ni kueneza Kiswahili pande zote za Dunia kupitia uimbaji huo. Niyonzima ameeleza Taarabu ilivyopokelewa na kukubalika nchini Canada. Tazama hapa video kufahamu mengi zaidi #USIPITWE

Ni ajabu na kweli, Roboti afanya upasuaji wa macho kwa mara ya kwanza Uingereza
Rais Kenyatta, Mbowe watoa msaada kwa waathirika wa Tetemeko la Ardhi