Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Hersi Said na Msaidizi wake Rodgers Gumbo pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mazingisa wamejipa jukumu la kuongeza Morari kwa wachezaji wa klabu hiyo, baada ya kuanza Kambi ya Maandalizi ya mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Simba SC.

Simba SC na Young Africans zitakwaana Jumamosi (Mei 28), katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza zikiwa na kumbukumbu ya kugawana alama kwenye michezo miwili ya Ligi Kuu msimu huu 2021/22.

Young Africans ilianza kambi rasmi jana Jumanne ‘Mei 24’ mkoani Shinyanga, baada ya kumaliza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Biashara United Mara Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Jumatatu ‘Mei 23’.

Kikawaida viongozi hao ni adimu kukutana kambini lakini Hersi amesisitiza kwamba kwa hali ilivyo lazima wakaze kila kona kwani Jumamosi ‘Mei 28’ wana jambo zito na la heshima kwenye Uwanja wa CCM Kirumba dhidi ya Simba SC.

Simba SC imeweka Kambi wilayani Misungwi, na inafanya mazoezi yake katika Uwanja wa Gwambina Complex unaomilikiwa na klabu ya Gwambina inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

Simba SC ilitinga Nusu Fainali ya ASFC kwa kuichapa Pamba FC mabao 4-0, huku Young Africans ikiitoa Geita Gold FC kwa changamoto ya Penati baada ya kutoshana nguvu ndani ya dakika 90.

Msajili apigilia msumari hukumu ya akina Mbatia
Ambundo, Ntibazonkiza watimuliwa Young Africans