Wamiliki wa Hotel za kitalii zilizoko katika fukwe mbalimbali nchini wamepigwa marufuku kutoza wananchi kiingilio wanapoenda kupumzika na kuogelea katika fukwe hizo.

Marufuku hiyo imetolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Mwanasheria wa NEMC, Manchari Heche alisema kuwa kwa mujibu wa sheria, fukwe zote ni mali ya umma hivyo hakuna anayepaswa kuzitumia kwa biashara akiwatoza fedha wananchi.

“Fukwe zote ni mali ya umma kwa sababu kuna mipaka yake, hivyo kitendo cha kuwatoza wananchi fedha kuingia katika fukwe hizo ni kosa kisheria na wanaofanya hivo wanapaswa kuacha mara moja,” alisema Heche.

Baadhi ya hotel zilizoko katika fukwe hususan jijini Dar es Salaam zimekuwa zikitoza wananchi kiingilio cha kati ya shilingi 10,000 na 40,000 kwa kutembelea fukwe hizo kupunga upepo na kuogelea.

Katika hatua nyingine, Heche aliwataka wawekezaji wote waliojenga katika fukwe za bahari kuhakikisha wako umbali wa mita 60 kutoka Baharini, kinyume cha hapo nyumba na hotel zao zilizo chini ya umbali huo zitabomolewa.

 

IGP Apangua Jeshi la Polisi, Wadai Haina Uhusiano na Kasi ya Magufuli
Profesa Maghembe: Mniamini Mimi