Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila Nyamadzabo ofisini kwake jijini Dodoma.

Mulamula amesema mazungumzo yake na Dkt. Taufila ambaye pia alikuwa anajitambulisha yamelenga kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Tanzania ili kuimarisha mahusiano hayo na hivyo kunufaika na miradi ya maendeleo.

Balozi Mulamula amesema Tanzania imejipanga kuhakikisha mahusiano kati ya Tanzania na Benki hiyo yanaimarika na kuendeleza uwezo wa watanzania wanaosimamia miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Benki ya Dunia ikiwa ni pamoja na kuendeleza sekta binafsi na kuifanya kuwa imara.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji hBenki ya Dunia Kanda ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila amesema miongoni mwa mambo waliyojadili leo ni pamoja na umuhimu wa kuhusisha sekta binafsi na kuiendeleza.

“Miongoni mwa vipaumbele vya Benki ya Dunia kwa sasa ni kuimarisha Sekta binafsi na kuifanya kuwa imara hasa katika maeneo ya biashara na uwekezaji pamoja na kuimarisha miundombinu ya usafirishaji, na ukuzaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano ili kuiwezesha duniani kuendelea kufanya shughuli zake hasa katika kipindi hiki cha changamoto ya ugonjwa wa Covid 19”. Amesema Dkt Taufila.

Agizo la Waziri kwa TFNS, MUHAS, SUA na TBS
Kiongozi mbio za mwenge agoma kufanya ufunguzi wa zahanati