Rais wa Rwanda Paul Kagame amemfuta kazi waziri wake wa afya Dkt. Agnes Binagwaho. Waziri huyo aliongoza wizara hiyo kwa kipindi cha miaka 5.

Dkt. Binagwaho alikuwa miongoni mwa mawaziri vigogo katika serikali ya Rwanda lakini inasemekana huenda aamefukuzwa kazi kutokana na utendaji kazi usioridhisha na matatizo yanayoikumba wizara hiyo kwa sasa.

Wakati wa mkutano wa kitaifa mwezi Desemba mwaka jana ,waziri huyo alikosolewa vikali na washiriki waliobainisha tatizo kubwa la ugonjwa wa malaria.

Katika kipindi cha miezi sita pekee ya mwaka huu wamehesabiwa wagonjwa milioni 1.,4 idadi ambayo ni kubwa sana ikilinganishwa na miaka 5 iliyopita ambapo Rwanda ilikuwa miongoni mwa mataifa yaliyokuwa katika nafasi nzuri ya kuangamiza ugonjwa huo.

Tatizo lililobainishwa na wakosoaji ni uzembe uliofanywa na wizara ya afya iliyoagiza vyandarua visivyotimiza viwango vya ubora na kugharimu wizara hiyo dolla milioni 15 za Marekani.

Katika ripoti ya mkaguzi mkuu wa mali ya umma,wizara ya afya ilibainisha pengo la milioni 10 dollar za Marekani zilizotoweka.

 

Rais Magufuli Awataka Wakurugenzi Kuwa Watatuzi wa Kero
Video: Dkt. Mwaka, Mandai na Fadhil wa Fadhaget Clinic Wafutiwa usajili na Wengine Wapewa Onyo