Waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Lawrence Masha (kulia pichani), alikamatwa jana baada ya kutofautiana na amri ya polisi katika kituo cha polisi cha Oysterbay, Dar es Salaam.

Taarifa zinaeleza kuwa Masha alikamatwa na kufungiwa ndani ya selo za Polisi kwa madai ya kuvunja sheria kwa kulazimisha kuwadhamini baadhi ya vijana wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema.

Vijana hao takribani 18 walikamatwa kwa tuhuma za kufanya maandamano  yasiyo rasmi wakiwa wamevalia fulana zenye jumbe mbalimbali za vyama vinavyounda Ukawa.

Hatima ya Lawlence Masha amabaye hivi karibuni alitangaza kuihama CCM na kujiunga na Chadema inatarajia kuanza kufahamika leo atakapofikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Zitto Kabwe Awashukia Wasanii Wanaopigia Debe Chama
Lowassa, Duni Haji Wamshitaki Mkapa Kwa Wananchi