Taarifa rasmi zinasema kwamba mabingwa wa Tanzania bara, Dar es salaam Young Africans wameamua kuwapeleka kwa mkopo wachezaji wake watatu ambao tayari wameshapata timu za kuchezea msimu ujao.

Wachezaji hao ni Hussein Javu anayejiunga na timu iliyorejea ligi kuu Maji Maji FC, ‘Wanalizombe’
Kiungo wa klabu hiyo Hassan Dilunga anakwenda kujiunga na Stand United ya Shinyanga, wakati mlindi wa kushoto, Edward Charles anatua kwa maafande wa JKT Ruvu.

Kibarua Cha Nigel Pearson Chasitishwa
Vanessa Mdee Aeleza Jinsi Alivyosifiwa na ‘Jay Z’ Walipokutana