Rais wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Injinia Hersi Said amewatoa hofu na wasiwasi Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo kuhusu mustakabali wa Kocha Mkuu Nasreddine Nabi.

Hersi amefunguka ishu hiyo, kufuatia tetesi kueleza huenda Kocha huyo kutoka nchini Tunisia akaondoka mwishoni mwa msimu huu, baada ya kumaliza mkataba wake ambao aliusaini mwanzoni mwa msimu huu.

Akizungumza kupitia Wasafi FM leo Jumatatu (Juni 05), Rais wa Young Africans Hersi Said amesema: “Niwatoe Wasiwasi , Nabi is here to stay. Kila mtu ana mkataba ambao una mwanzo na mwisho, mkataba wake unaisha msimu huu , lakini tumeishafanya nae mazungumzo ambayo yapo kwenye hatua za mwisho”

Katika hatua nyingine Kiongozi huyo amefunguka kuhusu mustakabali wa Beki wa kati kutoka visiwani Zanzibar Ibrahim Bacca ambaye amekuwa kigigi mujaraab kwa timu pinzani tangu alipoanza kupewa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Young Africans.

Hersi amesema Beki huyo ameshasaini mkataba mpya ambao unamuwezesha kulipwa fedha nyingi klabuni hapo, hivyo amewasisitiza Mashabiki na Wanachama kuendelea kumpa ushirikiano Bacca waliyemsajili msimu uliopita akitokea KMKM ya kwao Zanzibar.

“Hii ni Exclusive ambayo naitoa hapa. Ibrahim Bacca Tumemuongezea Mkataba na mshahara mkubwa. Siwezi kuutaja hapa kwa sababu ni mkataba wa siri wa pande mbili” amesema Hersi

Majambazi waliopora Pikipiki wajikuta wakila Nyasi
Hersi Said: Nina uhakika USMA itaadhibiwa CAF