Wananchi wa Jimbo la Pandani lililopo Pemba Zanzibar wanafanya uchaguzi mdogo leo Machi 28, 2021.

Jimbo la Mpandani linafanya Uchaguzi wa Mwakilishi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwakilishi Mteule wa Jimbo hilo Abubakar Khamis Bakari kupitia Chama cha ACT Wazalendo kufariki dunia, usiku wa kuamkia Novemba 11, 2020.

Marehemu Aboubakar Khamis, aliyekuwa Mwakilishi mteule jimbo la Pandani

Marehemu Aboubakar Khamis alichaguliwa kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Pandani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 na alifariki Dunia kabla ya kuapishwa.

Maalim Seif Azzan, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa ACT Wazalendo Jimbo la Pandani na Mpigakura wa Jimbo hilo akitoka kupiga kura katika kituo cha Skuli ya Pandani

Uchaguzi huo unashirikisha wagombea kutoka vyama mbalimbali vikiwemo vyama vya AAFP, ACT- Wazalendo, NLD, CCM, ADA-TADEA, ADC, CUF, MAKINI, NRA na UPDP.

Zoezi la kupiga kura Pandani linaendelea.

Rais Samia amsimamisha kazi Mkurugenzi mkuu TPA
Rais Samia kupokea ripoti za CAG, TAKUKURU leo