Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ametangaza kujiuzulu nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kufuatia tuhuma za rushwa zinazoikabili kamati hiyo.

Zitto amesema kuwa tayari ameshamuandikia barua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzani, Job Ndugai kumtaka achukue hatua kali dhidi ya wajumbe wa kamati wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

“Kuna tuhuma za rushwa dhidi ya Kamati mbalimbali za Bunge ikiwemo kamati ninayohudumu. Nimemwandikia Spika Kuomba Uchunguzi juu Ya tuhuma hizo na kwamba achukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayekutwa kuhusika na vitendo vya rushwa. Nimejiuzulu Ujumbe wa Kamati ili Kutoa Nafasi Ya Uchunguzi Husika,” Zitto ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Katika post nyingine, Zitto amesisitiza kuwa kitendo cha Spika wa Bunge kuwabadili wajumbe wa kamati za Bunge hakutoshi badala yake alipaswa kuanzisha uchungunguzi kubaini waliohusika na vitendo vya rushwa ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.

Amesema kuwa Bunge linapaswa kudumisha uadilifu zaidi ya kitu chochote. Aliongeza kuwa  kupokea au kutoa rushwa/hongo ni kosa la jinai na wabunge hawako juu ya sheria.

“The Speaker has just shuffled parliamentary committees by moving members from one committee to the other and some losing their leadership positions following bribery accusations. Parliament NEEDs to maintain its integrity above all else. I call for more investigations and a more comprehensive action by Speaker. Reshuffling is inadequate. Bribery is criminal and MPs are not above the law.”

Abdi Banda Aibuka Na Kukanusha Tuhuma Zinazomkabili
Petr Cech Mchezaji Bora wa Jamuhuri ya Czech