Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe ametoa sababu za kushuka kwa mapato ya Serikali na kusema kuwa Serikali inapaswa kutazama upya utendaji wake vinginevyo itabidi ikope ili kulipa mishahara kwa watumishi.

Amesema kuwa kwa miezi ya Julai na Agosti mwaka huu mapato ya serikali yalishuka mpaka shilingi 600 bilioni na kusema ni maporomoko makubwa hivyo madhara yake ni makubwa.

“Ni mporomoko mkubwa Sana na sio jambo la kushangilia hata kidogo. Madhara ya kushuka kwa mapato ni makubwa kwani mishahara ya watumishi wa Umma peke yake ni Shilingi 570 bilioni Kwa mwezi,”amesema Zitto

Hata hivyo, Zitto  ametaka serikali kutazama upya utendaji wake ili kuweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji nchini na kudai kama serikali haiatafanya hivyo itafika mahali itabidi ikope pesa ili kulipa mishahara ya watumishi mbalimbali

Spika wa Bunge ajiuzulu akipinga vitendo vya Serikali
Polisi yaanza uchunguzi kufuatia ajali ya moto