Upepo mkali wa kisiasa umezidi kukikumba Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambapo siku za hivi karibuni chama hicho kimezidi kukimbiwa na madiwa na wabunge ambao wamekuwa wakijiunga na Chama Tawala CCM.

Hali hiyo inaendelea, kwani aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ukonga kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mwita Waitara na mwenzie, Julius Kalanga Laizer wa jimbo la Monduli wamekihama chama hicho, huku kila mmoja akitoa sababu zake.

Tuhuma kubwa ambazo wamekuwa wakizitoa viongozi hao ni kukosekana kwa Demokrasia ndani ya chama hicho, hivyo kukosa uhuru wa kuhoji mambo mbalimbali ndani ya chama hicho.

Kufuatia hali hiyo, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete kupitia ukurasa wake wa ‘Twetter’ amewakaribishwa katika chama cha Mapinduzi, “Karibuni nyumbani kumenoga”.

Ridhiwani ameandika kuwa kama kuna wa kulaumiwa katika yanayoendelea basi ni mazuri yanayotekelezwa na Serikali ya CCM, kama hauwezi kupambana uungane nao (CCM),

Mahakama yalitoa MwanaHalisi kifungoni, lakutana na kiunzi kingine
Video: Nawasha moto wa kumchoma Mbowe, CCM inakotupeleka siko