Kituo cha uwekezaji hapa nchini kwa kushirikiana na taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) pamoja na jukwaa la biashara la india( IBF) na shirikisho la biashara la viwanda viwanda india( FICCI)  wameandaa kongamano la biashara  na uwekezaji  litalkalo fanyika siku ya jumapili tarehe 10/7/2016 kuanzia saa tatu asubuhi katika ukumbi wa Kilimanjaro hoteli

Hayo yamsemwa na meneja mahusiano wa kituo cha uwekezaji bw, Daudi Riganda  alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo,aidha alibainisha kuwa kongamano hilo linafanyika kufuatia ziara ya ktaifa ya Waziri Mkuu wa India Mh.Narendra Modi,anayetarajiwa kuwasili siku ya jumamosi tarehe 9/7/2016.

Lengo kuu la kongamano hilo ni kuwaleta pamoja wafanyabiashara wa india na Tanzania kukutana pamoja na kubadilishana uzoefu katka masuala ya biashara na uwekezaji,aidha ujumbe wa wafanya bishara kutoka India utajumuisha wafanya biashara kutoka katika sekta mabalimbali kama,Kilimo, Viwanda, Miundo Mbinu ,Elimu  ,Afya, Nishati na Maji.

Hata hivyo kulingana na takwimu za kituo cha uwekezaji Tanzania kati ya mwaka 1990 na juni 2016,kituo kimeweza kusajili jumla ya miradi442 ya uwekezaji kutika india yenye thamani ya dolla za kimarekani billion2.112.

Vilevile bw,Riganda aliongeza kuwa’’ miradi inayoongoza  katika kusajiliwa na (TIC) ni katika kipindi hiki ni ile iliyopo katka sekta ya viwanda na usindikaji, ambapo takribani asilimia53 ni miradi kutoka sekta hiyo’’

Umma wa wafanyabiashara kutoka Tanzania unakaribishwa na kudhibitisha ushiriki wao katika kongamano hilo la siku ya jumapili ili kuweza kushirikiana na wenzao kutoka nchi ya india ili waweze  kukuza ushirikiano.

Campus Vibez ya Times Fm kuwakutanisha vijana na Naibu Waziri Mavunde kesho asubuhi, Protea hotel
Nash MC afunguka kuhusu hali ya Fanani wa HBC baada ya kumtembelea ‘Rehab’