Mbunge wa Uganda ambaye inadaiwa aliteswa na maafisa wa usalama, Robert Kyagulanyi meruhusiwa kusafiri kuelekea Marekani kwaajili ya matibabu.

Alhamisi usiku Polisi walimkamata Kyagulanyi na mbunge mwenzake wa upinzani Francis Zaake uwanja wa ndege wa Kampala walipokuwa wanajaribu kutoroka nchini.

Aidha, Polisi walidai kuwa viongozi hao wa upinzani, ambao wote wanakabiliwa na tuhuma za uhaini walikuwa katika harakati za kukimbia.

Hata hivyo, wabunge hao wawili wamesema kuwa waliteswa baada ya kukamatwa huko nyuma na hospitali ya Kampala ilitoa pendekezo kwamba wapatiwe matibabu nje ya nchi.

 

 

Marekani yasitisha kutoa misaada kwa Palestina
Video: Ukatili wa kutisha Dar mgambo wa Makonda, CCM yawatosa wasanii kampeni 2020

Comments

comments