Katibu Muenezi wa CHADEMA Wilaya ya Kinondoni, George Mwingila amepinga vikali sababu zilizotolewa na aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia na kusema hazina ukweli wowote bali akubali kuwa njaa zake ndizo zilizomkimbiza.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa, Mtulia kuhama CUF ambayo ipo chini ya mwamvuli wa UKAWA kwa madai anakubali kazi zinazofanywa na Rais ni uongo mtupu kwani angeweza kumuunga mkono akiwa ndani ya chama chake na siyo kuhama.

“Kwenye ilani yetu ya uchaguzi tuliyoinadi mwaka 2015 hapakuwa na ajenda ya kubomolea watu nyumba zao na wala hatukuwa na ajenda ya kununua wanachama wa upinzani wala viongozi wake. Sasa unakuja kusema kwamba unamuunga mkono rais na chama chake, kwa nini usiseme wazi tu kwamba ni njaa zako zinakusumbua,”amesema Mwingila .

Aidha, amesema kuwa hata ndani ya Chadema wapo wanao muunga mkono Rais Dkt. Magufuli lakini hawana mpango wa kuhama chama.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa Wilaya ya Kinondoni ameongeza kuwa alichokifanya Mtulia ni Usaliti wa hali ya juu.

Majaliwa afanya ukaguzi wa makazi ya makamu wa Rais
Ujerumani yamuonya Trump kuhusu Jerusalem