Meya wa Ubungo, Boniface Jacob amewataka wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa watulivu kwani mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika yuko kwenye mikono salama hawezi kununulika kirahisi.

Ameyasema hayo mara baada ya kuwepo kwa taarifa zinazoenea kuwa mbunge huyo amejivua uanachama wa Chama hicho pamoja na nafasi yake ya Ubunge.

Aidha, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa mbunge huyo hawezi kununuliwa kama wanavyonunuliwa wengine na hakuna mtu wa kumshawishi kuhama chama.

“Mnyika siyo dizaini ya hao wanaopigiwa simu na kuahidiwa vyeo na madaraka ya kuhongwa, ni mbunge imara na anajua majukumu yake,”amesema Jacob.

 

Droo ASFC kufanyika ‘LIVE’ kesho
Serikali yawabana wamiliki wa nyumba