Katika harakati za Uchaguzi mkuu nchini Kenya, kinara wa ODM Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wanaelekea kufanya Muungano wa kisiasa kwenye safari ya kuingia Ikulu mwezi Agosti.

Inataarifiwa Kalonzo na Raila wako kwenye mazungumzo ya kuhakikisha kuwa wanaunda muungano utakaomwacha naibu rais William Ruto kinywa wazi ikiwa wawili hao wana timu ambazo zinaendeleza mashauriano na tayari masuala kadhaa yameafikiwa.

Mazungumzo hayo yalianza baada ya Rais Uhuru Kenyatta kukutana na wawili hao kwa siri na kuwataka kuungana ili waweze kupambana na muungano wa Kenya Kwanza.

Kalonzo ataingia vuguvugu la Azimio la Umoja kupitia OKA ambao ni muungano wa Narc Kenya ya Martha Karua, Kanu yake Gideon Moi na Cyrus Jirongo.

Wakati hayo yakiendelea, Maswali yameibuka kuhusu mahali alipo naibu rais William Ruto baada ya kukosa kuhudhuria mikutano na wenzake Musalia Mudavadi na Moses Wetangula.

Kabla ya kuingia mafichini, DP alikuwa akifanya mikutano kadhaa kila siku ili kuuza sera za mfumo wake wa Bottom up, hata hivyo kufikia sasa hajahudhuria kampeni mbili ambazo Mudavadi na Wetangula walifanya jijini Nairobi na pia Naivasha.

Frank Komba kumsaidia Tesema Ligi ya Mabingwa Afrika
ASEC yaipeleka Simba SC Benin