Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Atashasta Nditiye, amewataka wazazi pamoja na walezi kutoa ushirikiano mkubwa kwa walimu kwaajili ya malezi na makuzi ya watoto wao katika kipindi hiki cha likizo.

Amesema hayo wakati akitoa hutuba yake katika mahafali ya shule ya Kakangaga Muslim Sekondari iliyopo wilayani Kibondo mkoani Kigoma.

Amesema kuwa ataendelea kushirikiana na shule hiyo pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo wamiliki wa shule huku akiahidi January mwakani kukabidhi mifuko 100 ya Saruji kwaajili ya ujenzi unaonedelea wa vyumba vitatu vya madarasa na kutafuta namna nzuri ya kujenga uzio wa shule hiyo.

Kwaupande wake mkuu wa shule hiyo Sheikhe Abduljalilu Siraji ameushukuru uongozi wa wilaya ngazi ya wilaya na mkoa kwa kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa na kuitambua shule hiyo kwa kutoa mchango mkubwa wa elimu maana imebeba taswira ya mkoa wa Kigoma.

Akisoma taarifa ya shule kwenye mahafali ya 9 ya shule ya hiyo yaliyofanyika Desemba 05, mwaka huu, makamu mkuu wa shule hiyo Mwalimu, Fahad Zaidi amesema kuwa wamekuwa wakikumbana na changamoto ya wanafunzi wanapotoka likizo kuwa wamebadirika kitabia na mienendo.

Ameeleza kuwa changamoto hiyo ni moja ya changamoto mbaya Sana ambayo huweza kuwarudisha wanafunzi nyuma kitaaluma licha yakuwa wametoka shuleni wakiwa sawa.

Marekani: Gavana wa Georgia ashinikizwa kupindua uchaguzi
Boeing 737 MAX rasmi yarejea angani