Otile Brown na meneja wake Joseph Noriega wameamua rasmi kusitisha makubaliano ya kufanya kazi pamoja, ikiwa ni baada ya ushirikiano mkubwa waliokuwa nao kwa takriban miaka sita ambao unatajwa kuwa chachu ya mafanikio makubwa kwa mwimbaji huyo kutoka nchini Kenya.

Taarifa ya kutengana kwa wawili hao imechapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za mwimbaji Otile ikithibitisha mwisho wa wawili hao kikazi licha ya mafanikio makubwa yaliyotokana na ushirikiano kati yao.

Akitoa shukrani zake kwa meneja huyo, Otile Brown amekiri jukumu muhimu ambalo Joseph Noriega alilibeba katika kazi yake, akisema kwamba Noriega alichangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wake katika muziki.

“Kufanya kazi na Noriega kumekuwa tukio la ajabu. Mapenzi yake na usaidizi wake umekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wangu kama msanii. Nitathamini ushirikiano wetu milele,” alisema.

Mafanikio ambayo Otile Brown amepata katika maisha yake yote yanatumika kama ushahidi wa mchango mkubwa wa Joseph Noriega kwenye safari yake ya muziki. kwa pamoja, waliingia kwenye tasnia, wakatengeneza nyimbo zilizovuma na kumtambulisha Otile Brown rasmi katika tasnia ya muziki Tanzania.

Ange Postecoglou: Heshima ya Spurs inarudi
TPA yafafanua minong'ono uuzwaji Bandari ya Dsm Dubai