Kumbu kumbu ni muhimu sana katika maisha, haijalishi kama itakuwa inaumiza au inafurahisha. wengi hupenda zile zinafurahisha lakini zote ni kumbukumbu.

Mwisho wa wiki hii ulikua na matukio mbali mbali hapa nchini na yakiwa katika maeneo tofauti. Yapo matukio ambayo kwa namna moja au nyingine lazima yatabaki kama kumbukumbu. Haya ni baadhi ya matukio mwisho wa wiki hii:-

1. Rais Magufuli kukabidhiwa Uenyekiti wa CCM.

Ilikuwa ni kumbukumbu nzuri siku ya juma mosi ya tar 23 pale ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipitishwa kuwa Mwenyekiti baada ya kura zote za ndio kuelekezwa kwake tukio hilo lilifanyika Mkoani Dodoma. Rais Magufuli amempokea madaraka raisi Mstaafu Mh. Jakaya Kikwete.ccm magu

2.Mohammed Dewji kugawa nusu ya utajiri kusaidia jamii

Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL Group), Mohammed Dewji, ameungana na matajiri wakubwa duniani, kutangaza azma ya kugawa nusu ya mali zake kusaidia jamii.

Mtandao mashuhuri wa Forbes, umemkadiria Dewji kuwa anamiliki mali zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.1, akiongoza kundi la makampuni ya METL nchini Tanzania, linalojihusisha na biashara za viwanda vya nguo, vinu vya unga na viwanda vya mafuta ya kula, huku kinywaji chake cha Mo Cola, kikiuzwa bei rahisi

Mohammed-Dewji

3. Waliokuwa wanachama wa CCM kureje kutoka CHADEMA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida na baadaye kuhama chama na kujiunga na CHADEMA, Mgana Msindai ametangaza kurudi CCM juzi mjini Dodoma baada ya kupewaw nafasi na mwenyekiti Mstaafu Dkt Mrisho kikwete.

Msindai alisema aliamua kurudi CCM baada ya kuona kuwa sasa hakuna cha kupinga baada ya Rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais wa nchi, Msindai alihamia Chadema mwaka jana baada ya alialiyekuwa mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa kujiunga na Chadema mwaka jana wakati wa uchaguzi mkuu.

Pamoja na tukio la Msindai muigizaji Jackiline Wolper ambaye alimuunga Mkono Mh. Edward Lowassa kipindi cha uchaguzi mkuu naye alirudi ndani ya chama hicho akidai alikuwa amepotea na sasa amerudi kundini

dar

w

4.Kifo cha Askari wa Usalama barabarani

Taarifa za kifo cha askari wa usalama wa barabarani wa kituo cha polisi Oysterbay Dar es salaam kilichotakea  baada ya kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu wakati akiwa kazini katika eneo la Sayansi Kijitonyama zilianza kusambaa julai 22.

Taarifa zilizosambaa mitandaoni zilianza kumuhusisha  Askari mwingine wa barabarani aitwae Ashraf Shaban (pichani) ambaye wengi ndio wamezoea kumuona kwenye eneo hilo, lakini Kamanda wa polisi Simon Sirro alimtaja kwa jina moja tu kuwa aliyeuawa ni Sajent Mensah aliiambia Ayo tv

Chid Benz aeleza jinsi alivyomtoa machozi Mr Blue
Waziri Mkuu Kuhamia Dodoma Septemba Mwaka Huu