Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania – TPA, Plasduce Mbossa amesema Serikali haijasaini mkataba wa miaka 100 kwa ajili ya kukodisha Bandari ya Dar es Salaam.

Akiongea na kituo cha Clouds TV, Mbossa amesema pia Serikali haijaiuza Bandari hiyo kwani ina malengo mazuri na Bandari na kwamba TPA itahakikisha inaendeleza malengo mazuri ya shughuli za bandari kwa maslahi mapana ya nchi.

Amesema, “mtu anapokwambia Bandari imeuzwa lazima akueleze uratatibu, hiyo imeuzwaje uzwaje? Kwamba mtu anaondoka nayo, au anamiliki. Kwa hiyo ni seme hakuna swala la kuuza bandari.”

Mbossa ameiongeza kuwa, “kitakachofanyika ni kumwambia mwekezaji boresha, weka mitambo, hakikisha meli zinakaa masaa 2 badala siku 9 na vitu vingine vingi. Unamkodisha eno la kufanyia shughuli hizi za kibandari.”

Amesema, “na hilo tumekua tukilifanya – mfano kuna kampuni ya Hutchison kutoka Hong Kong ambayo imekua iki operate hapa kwetu kama TICTS – imekaa kwa miaka 22 – haikua imeuziwa bandari na ndio sababu imeondoka Disemba 2022 – walikua wamekodishwa.”

Rasmi Feisal Salum aondoka Young Africans
Mkude amuweka njia panda Kocha Simba SC