Serikali haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususani ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.

Hayo yamesemwa wilayani Mwanga na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina alipozindua rasmi oparesheni maalum ya uvamizi  na utambuzi wa mifugo.

Amesema kuwa uvamizi wa mifugo hiyo tokea nchi jirani ya Kenya unaleta changamoto kubwa ya malisho ya mifugo ya ndani ya nchi unaopelekea migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji na husababisha mmomonyoko wa udongo  na uharibifu wa mazingira.

“ Haiwezekani ng’ombe wanaingia kwa makundi makubwa hivi nchini na watendaji wa serikali wapo, lazima kutakuwa na shida katika utendaji, oparesheni hii itakuwa ni ya mwisho, kwa ng’ombe watakaoingia tena watendaji watatolewa sadaka.”amesema Luhaga.

Hata hivyo, wataalam waliyokuwepo katika oparesheni hiyo maalum waliezeza kuwa mifugo mingi iliyoonekana kutokea angani ilikuwa zaidi katika maeneo ya malisho na maji ya vijiji vya kiti cha Mungu,njiapanda,kirya na kitongoi cha Mangulai.

 

Tanzania na Kenya zashuka viwango vya FIFA, Ujerumani, Brazil za paa juu
Nakumatt ya Mlimani City yafungwa