Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Daniel Chongolo amepokea malalmiko ya Wananchi wa Kijiji cha Ndaleta kilichopo Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, juu ya kero ya Wanyamapori hususani Tembo wanaovamia makazi na mashamba yao na kufanya Uharibifu wa Mali, Mazao.

Mbele ya Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere, Wananchi hao hii leo Machi 9, 2023 wametoa malalamiko hayo, mara baada ya msafara wa Katibu Mkuu Chongolo kusimama katika Kijiji hicho ukielekea Kiteto.

Wananchi wa Kijiji cha Ndaleta kilichopo Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara walipokuwa wakiwasilisha kero zao kwa Katibu Chongolo.

Kwa nyakati tofauti, mkazi wa Ndaleta Abdallah Mfaume na Mbunge wake Ole Sendeka wamemuomba Katibu Mkuu Chongolo kuishauri Serikali kuja na mkakati wa kuzuia uvamizi wa Tembo kwenye makazi ya Wananchi, ili waishi kwa amani na bila hofu ya Wanyamapori hao wanaotoka Hifadhi ya Tarangire.

“Ndugu Katibu Mkuu hapa katika eneo hili la Ndaleta na Vijiji vingine Jirani kumekuwepo na hofu kubwa ya Uvamizi Wanyamapori ambao licha ya Kuharibu makazi, Mashamba, mifugo na pia husababisha hata vifo vya Wananchi,” amesema Ole Sendeka.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Daniel Chongolo na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere walipokuwa wakizungumza na Wananchi hao.

Akijibu malalamiko hayo, Chongolo amesema atawaita Mawaziri wanaohusika na Wanyamapori ili kujua mpango wa kuwadhibiti wasiweze kuingia kwenye makazi ya Wananchi na ikiwezekana kuwe na mfuko wa fidia kwa Wananchi wanaoathiriwa.

“Wiki ijayo nitakutana na Mamlaka zinazohusika ikiwemo Mawaziri wanieleze kwa kina mipango yao kuhusiana na fidia ya athari za uvamizi wa wanyamapori hasa Tembo ambao wanaotokea Tarangire na Hifadhi zingine, lazima kuwepo na mfuko wa Fidia kwa ajili ya Uvamizi wa wanyamapori,” amesema Chongolo.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 10, 2023
Ujenzi Daraja la JPM Kigogo - Busisi wafikia asilimia 70