Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), kimetoa mchango wa rambirambi kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa chama hicho, Hashim Rungwe amesema kuwa wametoa rambirambi hiyo baada ya kuguswa na ajali hiyo.

Amesema kuwa wao kama Watanzania wana wajibu mkubwa wa kuweza kuchangia rambirambi kwa familia zilizofikwa na maafa.

“Sisi kama chama cha CHAUMMA, tumetoa mchango wetu kiasi cha shilingi laki tatu 300,000 ili ziweze kusaidia katika familia mbalimbali zilizofikwa na maafa,”amesema Rungwe

Ole Sendeka atuma salamu za rambrambi kwa JPM
Video: Prof. Lipumba adai yuko tayari kuachia ngazi

Comments

comments