Wakurugenzi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko – CPB, wamepigwa msasa kwa kupatiwa mafunzo ya kiuongozi ya Utawala Bora na Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania – IoDT.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza mara baada ya mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi CPB, Salum Awadh amesema wamefurahi kupatiwa mafunzo hayo yanayoendelea.

Amesema, mafunzo hayo waliyopata yatasaidia kuongoza kwa weredi na ufanisi mkubwa ikiwana na lengo la kukuza Uchumi wa Nchi na mtu mmoja mmoja.

‘’Kwenye mashirika ya umma kuna changamoto za kiungozi ya kusimamia mali za umma, hivyo ukiwa na uwezo mdogo huwezi kusimamia rasilimali, kwa hiyo mafunzo haya yatasaidia wakurugenzi wa Bodi kuelewa mipaka yao na kukabiliana na changamoto za kiungozi,’’ amesema Mwenyekiti huyo.

Aidha ameongeza kuwa, mafunzo yanasaidia kuonesha mipaka kati ya Bodi na Menejiment na kwamba yamekuja wakati muhafaka katika uongozi huo mpya, ili waweze kuonesha mabadiliko kwani awali Bodi hiyo ilikuwa ikifanya kazi zake kwa ufanisi mdogo lakini katika msimu huu Bodi hiyo imepanga kuboresha ufanisi wake kwa kuchakata mazoa zaidi ya tani 200.

Mwenyekiti huyo amesema katika kipindi cha nyuma katika upande wa viwanda walikua hawafanyi vizuri hivyo sasa wamejipanga kufanya kwa ufanisi kutoka asilimia 30 hadi kufikia asilimia 70.

Naye mmoja wa wajumbe wa Bodi hiyo, Kapenjama Ndile alisema mafunzo hayo yatawasaidia kuendesha mashirika ya umma kwa kuongeza uwezo wa kiulewa wa namna ya kuendesha mashirika ya umma hasa katika sekta ya Kilimo.

‘’Tuko hapa Mwanza leo siku ya Tano tunanolewa na magwiji wa mafunzo tunaamini wazi tukitoka hapa tunaenda kufanya mapinduzi makubwa ya kiungozi katika Bodi ya CPB’’, amesema Ndile ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea.

Taasisi ya IoDT imekuwa ikitoa mafunzo katika kipindi cha wiki Nzima Jijini Mwanza kwa Wakurugenzi wa taasisi mbalimbali za umma wakiwemo Wakurugenzi wa Bodi ya CPB, ambao wamepatiwa mafunzo ya uongozi na Utawala Bora.

Kwa upande wa CPB, lenyewe ni Shirika la Umma la Kibiashara lililopo Chini ya Wizara ya Kilimo ambalo ununua mazao kutoka kwa Wakulima na wafanyabiashara wa Mazao na kuyaongezea thamani kwa kuyachakata katika viwanda vyao vilivyopo katika baadhi ya Mikoa Nchini.

Mbwana Makata aweka wazi mapugufu Ruvu Shooting
Sadio Mane azigonganisha klabu za England