Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa amesema zoezi la kuhamishia Wananchi Msomera Mkoani Tanga kutoka Hifadhi ya Ngorongoro linaendelea na halijasimamishwa kama inavyosemekana.

Mchengerwa ameyasema hayo jijini Dodoma, na kuongeza kuwa baadhi ya majirani wamekuwa wakizusha kuwa zoezi hilo limesitishwa kitu ambacho si cha kweli.

Amesema, “niwaahidi wananchi waliosalia na ambao wamekuwa wakijiandikisha kwa wingi na kwa shauku kutaka kuhama kuwa zoezi hili bado halijasimamishwa na Serikali, tofauti na inavyosemekana kwa baadhi ya wanaojaribu kukwamisha.”

Aidha, ameongeza kuwa, “Serikali imejiandaa na ina rasilimali za kutosha za kukamilisha zoezi hilo na haitarudi nyuma wala hakutakuwa na kusalimu amri katika kukamilisha zoezi hili ambalo litaendelea kufanyika kwa weledi na kasi kubwa.

Asensio huyooooooooo PSG
Robertinho afunguka saa 120 Simba SC