Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC leo itakosa huduma ya nahodha na mshambuliaji, John Bocco ambaye ni majeraha pamoja na kiungo Jonas Mkude.

Wawili hao kwa muda wa majuma kadhaa wamekosa kuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC, ambapo kwa upande wa Bocco amekua majeruhi kwa muda mrefu, lakini Mkude kabla ya kuingia kwenye orodha ya wachezaji majeruhi alikua anatumikia adhabu kufautia utovu wa nidhamu aliouonesha mwishoni mwa mwaka 2020.

Wakati wawili hao wakitarajiwa kuukosa mchezo wa leo dhidi ya Biashara United Mara, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Simba SC Haji Manara amesema wamejipanga vizuri na wapo tayari kupata matokeo mazuri ndani ya Uwanja wa Karume, mkoani Mara.

“Kila kitu kipo sawa na tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu ila tunahitaji pointi tatu ndani ya uwanja.” Amesema Manara.

Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kutokana na mipango ya makocha kuhitaji ushindi.

Kocha Mkuu wa Biashara United Mara Francis Baraza, anahitaji kulipa kisasi cha kufungwa mabao 4-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salam.

Kwenye mchezo huo mshambuliaji wa pembeni kutoka Msumbiji, Luis Miquissone aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kupiga asisti tatu ‘HAT TRICK’.

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema anahitaji alama tatu za mchezo wa leo ili kupunguza pengo la alama saba anazodaiwa na Young Africans inayoongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na alama 46 baada ya kucheza michezo 20.

Simba imecheza michezo 17 ina alama 39 ikiwa nafasi ya pili msimu wa 2020/21.

Julio atoa sababu za kupigwa 4G
Huyu ndiye Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi