Kiungo Mshambuliaji kutoka England Alex Oxlade-Chamberlain ana onekana kukosa chaguo linapokuja suala la kuchagua wapi atakapocheza msimu ujao 2023/24, ikiwa ataondoka Liverpool.

Chamberlain mwenye umri wa miaka 29, alijiunga na Liverpool mwaka 2017 akitokea Arsenal, lakini ameshindwa kuleta matokeo ya kudumu pale Anfield na mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Mchezaji huyo ambaye tayari ameshaitumiki England katika michezo 35, amekuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa Ubingwa wa Ulaya na Ligi Kuu ‘EPL’ lakini mara chache amekuwa akishindwa kumaliza dakika 90.

Majeraha yamemweka nje ya uwanja kwa muda mwingi wa msimu wa 2022-23.

Kwa mujibu wa gazeti la The Daily Mail, Klabu za Brighton, Newcastle na Aston Villa zinatajwa kumuwania mchezaji huyo mwishoni mwa msimu huu, ambapo atakuwa mchezaji huru.

Meneja wa Newcastle Eddie Howe ameripotiwa kumtaka mchezaji huyo mzaliwa wa Portsmouth huku Magpies hao wakipania kuunda kikosi kitakachoweza kushinda taji hilo ndani ya miaka michache ijayo.

Brighton imekuwa ikihusishwa vikali na nyota huyo wa zamani wa Arsenal, lakini wakasitishwa Januari kwa mpango, unaosemekana kuwa tayari kumchukua Oxlade kama kuchagua kujiunga na Villa ya Unai Emery kule Midlands.

Matariji wapishana kuinunua Man Utd
Young Africans matumaini kibao Lubumbashi